Kenya inakabiliwa na changamoto upya kuhusiana na sheria ya kukabili matumizi ya madawa ya kututumua misuli miongoni mwa wanariadha wake.
Licha ya nchi hiyo kupitisha sheria mwezi uliopita iliyowezesha kubuniwa kwa halmashauri ya kupigana dhidi ya madawa yaliyopigwa marufuku, kamati ya nidhamu ya shirikisho la kupambana na madawa yaliyopigwa marufuku duniani WADA inasisitiza kuwa sheria hiyo haikuafikiana na mapendekezo ya WADA.

Kamati hiyo inapendekeza kuwa hatua ichukuliwe dhidi ya Kenya kwa kujumuisha vipengee fulani ambavyo vinakinzana na kanuni za WADA.
BBC imebaini kuwa halmashauri kuu ya WADA itakubali mapendekezo hayo katika mkutano wao mkuu baadaye leo mjini Montreal Canada.
Iwapo hilo litatekelezwa basi itakuwa wajibu wa kamati ya olimpiki duniani IOC kuipiga marufuku Kenya kutoshiriki mashindano yake hadi pale itakapotekeleza masharti iliyowekewa.
WADA ilikuwa imeipa Kenya makataa mapya ya hadi Mei 2 kuidhinisha sheria hiyo la sivyo ikabiliwe na hatari ya kuadhibiwa.
Image copyrightEPA
Image captionTakriban wanariadha 40 wameadhibiwa na shirika la riadha duniani (IAAF) kwa kupatikana wakiwa wametumia dawa hizo tangu mwaka 2012.
Mswada huo mpya unaharamisha matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuweka mikakati ya kukabiliana na wanaohusika ilipitishwa na kuwa sheria na rais Uhuru Kenyatta.
Takriban wanariadha 40 wameadhibiwa na shirika la riadha duniani (IAAF) kwa kupatikana wakiwa wametumia dawa hizo tangu mwaka 2012.
Bingwa mtetezi wa mbio za Boston marathon na Chicago pia ni miongoni mwa walioadhibiwa.
WADA ilikuwa imetoa masharti makali ya kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwili, pamoja na kutolewa kwa ufadhili wa kila mwaka wa $50,000 milioni kwa idara ya kukabiliana na tatizo hilo.
Tatizo la dawa zilizoharamishwa Kenya
Image copyrightB
Image captionBingwa mtetezi wa mbio za Boston marathon na Chicago Ritah Jeptoo pia ni miongoni mwa walioadhibiwa.
Kufikia 2011, zaidi ya wanariadha 40 walikuwa wamepatikana wametumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Kufikia Januari 2016, wanariadha 18 wa Kenya walikuwa wanatumikia marufuku
Wanariadha hao 18 walikuwa wanatumikia marufuku ya jumla ya miaka 55
Maarufu zaidi ni Rita Jeptoo, mshindi wa marathon za Boston na Chicago Lilian Moraa Mariita anatumikia marufuku ndefu zaidi – miaka minane.