Serikali ya Rwanda imesema kuwa haijawafukuza wakimbizi kutoka Burundi na kwamba wanaofukuzwa ni raia wa Burundi wasio na vibali vya kuishi nchini humo.
Gavana wa jimbo la kusini mwa Rwanda ambako zaidi ya warundi 1000 wamekwishatimuliwa ameiambia BBC kwamba wanaofukuzwa walitakiwa kupata vibali vya kuendelea kuishi nchini humo na kisha warejee ikiwa watapenda.

Rwanda na Burundi hazijakuwa na uhusiano mzuri katika siku za hivi karibuni baada ya Burundi kuushutumu utawala wa kigali kwa kushirikiana na waasi kujaribu kuungoa utawala wa rais Pierre Nkurunziza.