Waziri wa Ulinzi wa Marekani , Ash Carter ametoa wito kwa Urusi kuachana na mfumo wake wa kutatua migogoro kwa kutumia nguvu huku akionyesha wasiwasi wake kuhusu kile alichokiita mpango wake wa vitisho vya nyuklia.
Katika hotuba yake nchini Ujerumani,Carter alitetea uwepo wa vikosi vya jeshi la Marekani katika Ulaya ya Mashariki.Amesema kuwa Marekani haitafuti vita baridi dhidi ya Urusi,achilia vita moto,lakini ni lazima iwaunge mkono washirika wake.
Carter amesema kuwa Urusi ilionekana dhahiri kukiuka baadhi ya mikataba ya amani ya umoja wa mataifa inayoleta amani kwa dunia na Urusi pia kwa kukiuka uadilifu,uhuru na mipaka ya nchi za Ukraine,Georgia na Moldova.
0 Comments