Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyanganyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.
Alitoa tangazo lake punde tu baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana.Cruz amewaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila analoweza katika kampeni zake,lakini hakukuwa na njia ya yeye kuweza kusonga mbele zaidi.
Mwandishi wa BBC aliyepo katika vituo vya kupigia kura Indiana amesema wafuasi wa Cruz wamestushwa na kukatishwa tamaa.Tangazo hilo linatoa mwanya kwa Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican.
|
0 Comments