Timu ya kimataifa ya wanasayansi imekamilisha utafiti mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa maumbile ya saratani ya matiti, ambayo wanasema inawapa karibu picha kamili ya nini husababisha ugonjwa huo.
Wanasayansi hao wanajaribu kutizama mfuatano wa jinomu kamili wa kesi zaidi ya mia tano za saratani ya matiti.Utafiti huo unaoongozwa na taasisi ya Cambridge umeweza kugundua aina tano mpya za visababishi (seli) vya ugonjwa huo.
Utafutu huo walau unaweka wazi uhakika wa asilimia 93 kama seli hizi zikibadilika kuweza kusababisha uvimbe.Watafiti wanasema kuwa taarifa hizi zitaweza kusababisha kupatikana matibabu kamili kwa binadamu.
|
0 Comments