Polisi nchini Nigeria wamemkamata mwanamme mmoja kwenye mji mkuu Abuja, baada ya kugundua kuwa amekuwa akidanganya kuwa yeye ni daktari na kuwatibu wagonjwa kwa muda wa miaka 10.
Victor Moffat Akpan, analaumiwa kwa kufungua kliniki ya akina mama kujifungua akitumia stakabadhi bandia.
Anadaiwa kusaidia akina mama kujifungua na pia kufanya upasuaji.
Bwana Akpan, hajasema lolote kuhusu madai hayo na pia analaumiwa kwa kutumia namba ya usajili ya daktarii mwingine aliyehitimu mwaka 1995.
|
0 Comments