Jaji nchini Uganda ametoa amri kuwa kesi ya kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye, ifanyike mahakamani kwa makosa ya uhaini na wala sio kwenye gereza lenye ulinzi mkali ambapo anazuiliwa.

Besigye alifikishwa mahakamani kwa muda mfupi ambapo kesi yake iliahairisha hadi tarehe 29 mwezi Juni.
Mwendesha mashtaka aliomba kesi hiyo kufanyika mahakamani kutokana na sababu za kiusalama.
Alikamatwa mwezi uliopita na kushtakiwa kwa uhaini baada ya kupanga sherehe za kuapishwa kwake kama rais.
Alipinga ushindi wa Rais Yoweri Museveni wa awamu ya tano wa uchaguzi wa mwezi Februari.