Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 7, 2016

Hillary Clinton atimiza idadi anayopaswa

Hillary Clinton ameripotiwa kufikisha idadi ya wajumbe anayohitaji ili kupata uteuzi wa chama chake ya kuwania nafasi ya urais wa Marekani.
Idadi hiyo imefikiwa katika majumuisho yanayofanywa na wakala wa habari Associated Press.

Taarifa hizi zinakuja kabla ya kinyang'anyiro cha leo katika majimbo sita, ikiwemo California.
AP imesema idadi hiyo imefikiwa baada ya ushindi wa Clinton dhidi ya mshindani wake Bernie Sanders huko Puerto Rico mwishoni mwa juma na kuongezeka kwa idadi ya wajumbe ambao wanaruhusiwa kumuunga mkono mtu yeyote wanaemtaka.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP