Hillary Clinton anatarajiwa kuhutubia katika sherehe za ushindi mjini Brooklyn punde tu baada ya matokeo ya kura za awali yaliyofanywa katika majimbo sita siku ya Jumanne kutangazwa na kuthibitika kwamba yanamuongezea nafasi yake ya kuteuliwa kuwa mgombea rasmi wa urais katika chama chake cha Democratic Party.

Kuna uwezekano wa yeye kugusia kuhusu uteuzi wake wa kihistoria kama mwanamke kutoka chama chochote cha kikubwa cha kisiasa nchini Marekani.
Wakala wa habari, Associated Press imesema Clinton tayari amefikisha idadi ya wajumbe wanaohitajika kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya wajumbe huru wenye mamlaka ya kumuunga mkono mgombea yoyote.Kampeni yake hivi sasa imejikita zaidi katika kumshawishi mpinzani Bernie Sanders kukubali kushindwa ili kusaidia kuunganisha nguvu ya chama kwa ajili ya uchaguzi ujao.
Wakati huo huo, anaetarajiwa kupeperusha bendera chama cha Republican amesema kauli yake kuhusu hakimu kwenye asili ya Mexico na Marekani kwamba imeeleweka vibaya.
Donald Trump amesema hakimu huyo hawezi kutoa hukum ya haki kwa sababu ana asili ya Mexico.
Paul Ryan, ambae ni spika wa bunge la Marekani amemtuhumu Trump kwa kauli zake za kibaguzi.
Paul Ryan, ambae amemuunga mkono Trump wiki iliyopita, amemtaka kufuta kauli yake.