Waziri Mkuu wa Uingereza na mpinzani wake anayetaka Uingereza kujitenga na Muungano wa ulaya, Nigel Farage, wameulizwa maswala makali kuhusu athari za Uingereza kujiondoa kwenye muungano huo wakati wa mdahalo wa Runinga.

Bwana Cameron alirejelea hoja yake kuwa uchumi wa taifa hilo utasambaratika ikiwa kura hiyo ya maoni itaidhinishwa. Lakini Bwana Farage kwa upande wake amesema wataalamu wa kiuchumi wanao onya dhidi ya uingereza kujiondoa hawasemi ukweli.