Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 9, 2016

Jeneza la Muhammad Ali laswaliwa Marekani

Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani.
Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.
Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville.

AliImage copyrightGETTY
Image captionMuhammad Ali alifariki Ijumaa akitibiwa Arizona

Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani.
Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu.

MaelfuImage copyrightGETTY
Image captionMaelfu ya watu wamehudhulia swala hiyo

Mazishi yake yatafanyika Ijumaa.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP