Maelfu ya watu wanazidi kuingia barani ulaya kutoka nchini Eritrea kwa mwaka wa jana kuliko nchi nyinginge zote za Africa na taarifa hii ni kwa muujibu wa takwimu za umoja wa ulaya.

Nchi hii ndogo ya Eritrea, ambayo inakadiriwa kuwa na watu wapatao milioni tatu unusu,ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Ethiopia miaka ishirini na tano iliyopita,baada ya miaka thelathini ya vita.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, katika kipindi chote hicho hakukuwahi kufanyika uchaguzi, hakuna bunge, na hakuna uhuru wa vyombo vya habari.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiilaumu serikali kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu, ikiwemo mateso, kifungo cha jumuiya, utumwa na kwa muda mrefu kulazimishwa kulitumikia jeshi.