Mashirika kadha ya habari nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, yamesitisha matangazo yao kama njia ya kupinga kupanda kwa gharama ya Intenet inayotumiwa na simu za mkononi.

Simu za mkononi ndio hutumiwa na watu wengi zaidi kwa huduma ya internet nchini humo.
Baadhi ya watoa huduma ya mawasiliano ya simu wameongeza malipo kwa hadi zaidi ya asilimia 500 mwezi uliopita.
Chama cha mashirika ya habari nchini humo, kinasema kuwa hatua hiyo ni ukiukaji wa haki ya watu kupata habari.