Mataifa 6 waanzilishi wa Muungano wa Ulaya EU wanakutana leo kujadili mustakabali wao wa baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano huo.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy, Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo pasi na kuwa na ngoja ngoja.
Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU .

Image copyrightAP
Image captionViongozi wa Muungano wa Ulaya

Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala hilo likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ang'atuke kutoka madarakani baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni iliyoamua nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa Ulaya.
Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka muungano wa Ulaya...

Image copyrightAFP
Image captionJean Clauide Juncker na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amewatahadharisha wenzake kutokuwa na hamaki na kutaka kuchua hatua za kama kuilipizia kisasi Uingereza .
Ameomba kuwepo kwa subra na umakini katika kulishughulikia swala hilo ambalo anasema linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia mahitaji ya raia wa jumuiya ya muungano wa Ulaya.