Mwalimu mmoja wa shule ya msingi katika eneo la kati nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake.
Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaodhulumu watoto kijinsia nchini Kenya.
Mwalimu John Gichia Mugi 23 alishtakiwa kwa kuwabaka wavulana 10 wa shule ya msingi ya Muran'ga takriban kilomita 120 magharibi mwa Nairobi mwaka wa 2015.
Mwalimu huyo wa kujitolea atatumikia kifungo cha miaka 10 gerezani mfululizo kwa kila mmoja wa makosa hayo aliyopatikana na hatia.
Jaji alisema mwalimu walikuwa amesaliti dhamana na imani aliyopewa na wazazi wa wanafunzi hao wachanga ambao alipaswa kuwatunza

Image captionWavulana hao walikuwa na ushahidi kuwa Mugi aliwaguswa sehemu zao za siri na wakati mwingi anawabusu

Wavulana hao walikuwa na ushahidi kuwa Mugi aliwaguswa sehemu zao za siri na wakati mwingi anawabusu.
Wakati huo alikuwa akihudumu kama mwalimu anayesimamia maswala ya bweni katika shule yao ya msingi.
Kifungo hicho cha miaka 90 ni ishara tu kuwa sera za serikali ya Kenya imeanza kuchukua hatua kali dhidi ya wale wanaowadhulumu watoto nchini kenya.
Ikiwa atajaaliwa na maiasha marefu, Mugi ataachiliwa akiwa na umri wa miaka 113