Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 5, 2016

MOL FC BADO TISHIO UBELGIJI YAIBUGIZA ANTWERPEN FC KWAO 4-3

Kikosi kigumu na bora cha timu ya Mol kikipata picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.

Timu ngumu ambayo inaendeleza ubabe kila mara kwa timu zote za kiafrika nchini Ubelgiji Mol Fc jana iliendeleza vyema shughuli zake za kukata kilimilimi kwa timu zote zilizo na uwezo wa chini kimchezo kwa kuwafundisha Antwerpen Fc soka baada ya kuirarua kwa jumala ya goli 4-3 katika uwanja wa Antwerpen.


Mol ina kila sababu ya kuwa timu bora kwa kujidhihirishia jana pale ilipoifunga Antwerpen Fc ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.

Ikicheza kwa kujiamini zaidi Mol Fc ilicheza mchezo mzuri sana na kila mmoja aliyekuwepo uwanjani pale alikisifia kikosi hicho.Antwerpen hii ni mechi yao ya pili sasa kupoteza,kabla ya mechi ya jana ilibugia goli 5-3 toka kwa Mavetarani wa Antwerpen.

Mara baada ya mchezo kumalizika Uongozi wa Mol Fc ulitangaza kutaka mechi na vijana wa Holland kwani kwa hapa Ubelgiji timu zote kama Antwerpen, Leuven na Liege wote walishachezea vichapo kila walipokutana na Mol Fc.

Kikosi cha Antwerpen FC kikipata picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.

Wachezaji wa timu zote mbili wakipata picha ya pamoja kama kumbukumbu

Golikipa namba moja wa Mol ambaye ni majeruhi wa mkono Maganga One akitoa maelekezo kwa mshambuliaji wa Mol Fc Mohammed wakati wa mapumziko

Wachezaji wa Antwerpen FC wakijaribu kuelekezana jambo nini wafanye baada ya kuona Mol Fc wakilisakama lango lao bila kizuizi

Mchezaji Ndela ambaye jana alikasilishwa na uchezaji mbovu  wa timu yake ya Antwerpen,mchezaji huyo ambaye alidiriki kutoa siri za timu yao kwamba timu yake ilikodi wachezaji wengi na kusababisha timu yao kushindwa kucheza kwa maelewano hivyo kuipa nafasi Mol Fc kufanya wananvyotaka uwanjani.Mchezo wa jana Mol Fc iliifunga Antwerpen Fc uwanja wa nyumbani kwao Antwerpen jumla ya magoli 4-3

Baadhi ya wachezaji wa Antwerpen Fc wakijaribu kutafakari baada ya kukubali goli 3-2 mpaka kipindi ca kwanza kinaisha.Mchezo wa jana ulifanyika jijini Antwerpen ambapo Mol Fc ilifanikiwa kuifunga Antwerpen katika uwanja wao wa nyumbani jumla ya goli 4-3

Kutoka kushoto ni Dulla Criss Cross kiongozi wa Antwerpen Fc,katikati ni Golikipa namba moja wa Mol na mwisho kulia ni mchezaji wa Antwerpen Dulla G

Umoja ni Ushindi na hapo Mol ikijidhihirishia ushindi huo mara tu baada ya mpira kumalizika na kutoka uwanjani kifua mbele.Mol jana iliweza kfanikiwa kutumia vyema mechi yake ya kwanza ugenini baada ya kuifunga Antwerpen Fc jumla ya magoli 4-3.

Mmoja wa viongozi wa timu ya Mol,Yusuf kulia akiwa na mchezaji Kijoka Kikuku mara baada ya mchezo kumalizika.Mchezo huo wa jana uliochezwa jijini Antwerpen na matokeo timu ya Antwerpen kushindwa kuidhibiti timu ngumu ya Mol na kukubali kuvurugwa uwanja wao wa nyumbani kwa kuruhusu goli nne kwa tatu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP