Wachezaji wa Antwerpen wanaonekana wakiulaumu uongozi wa timu yao kwa kukodi wachezaji,mchezo mbaya,wachezaji kutoelewana na kulaumiana uwanjani.Vilevile walipeleka lawama zao kwa Mussa ambaye jana hali yake haikuwa nzuri mara baada ya kupokea habari ya timu yake kufungwa uwanja wao wa nyumban.Mussa kiongozi wa timu ya Antwerpen mwenye kelele nyingi ambazo huwa hazina makali pindi wakikutana na wababe wao Mol.Jana Mol ilituma salamu hizi kwa Mussa ambaye hivi karibuni ilisemekana alikimbilia Zanzibar kwa kuhofia aibu ya kichapo kilichowakuta jana.


Baadhi ya wachezaji wa Mol Fc wakionekana kushangilia ushindi wao mara baada ya mpira kumalizika.