Jumla ya watu wanane wameuawa baada ya kupigwa risasi ndani ya kambi ya kijeshi ya Makindye mjini kampala nchini Uganda
Msemaji wa jeshi la Uganda meja Edward Birungi, anasema kuwa mwanajeshi huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe.

Anaripotiwa kuwa mlevu na alikuwa pia amevuta bangi akiwa kazini, ambapo alianza kufyatua risasi kiholela akimtafuta mkewe ambaye alifanikiwa kutoroka.
Wanawake wanne akiwemo mwanajeshi waliuawa wakati wa kisa hicho.
Wengiwe waliouawa ni pamoja na wake wa wanajeshi wengine, wakiwemo pia watoto watatu.
Mwanajeshi hyuo naye aliuawa kwa kupigwa risasi.