Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini mwa uingereza.
Cox Ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini Uingereza tangu Ian Gow auawe mwaka 1990.
Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana.

Image copyrightGETTY

Walioshuhudia wanasema kuwa mbunge huyo aliingilia kati mzozo kati ya wanaume wawili eneo ambapo alikuwa akikutana na watu eneo lake la ubunge.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati.
Kisha muuaji akaanza kumchoma kisu alipokuwa amelala chini