Picha ya Mwanamfalme wa Uingereza William, imechapishwa katika ukurasa wa mbele wa jarida la wapenzi wa jinsia moja kuzungumzia dhuluma dhidi ya watu wenye maumbile hayo.
William aliambia jarida hilo la Atittude,kwamba watu wa jinsia moja wanastahili kufurahia jinsi walivyo.
Amekuwa mtu wa kwanza kutoka katika familia ya kifalme kukubali picha yake kuwekwa katika jarida linaloandika habari za wapenzi wa jinsia moja.
Mwanamfalme William alifungua rasmi mkutano mjini London mwezi uliopita ambapo aliweza kukutana na wapenzi wa jinsia moja na kuelezewa kuhusu dhuluma ambazo watu hao hukumbana nazo na jinsi zinavyowaletea madhara ya kiakili.
Mamake mwanamfalme huyo,Diana alijaribu kukabiliana na ubaguzi wa kijinsia kupitia misaada mbalimbali.
|
0 Comments