Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 15, 2016

Roboti kupokea wageni hospitalini Ubelgiji

Roboti kwa jina Pepper, iliyotengenezwa kuelewa hisia za watu inatarajiwa kuanza kazi mpya kama karani wa mapokezi katika hospitali mbili nchini Ubelgiji.
Roboti hiyo itakuwa ya kwanza kuhudumu katika jumba la matibabu baada ya roboti nyengine kuwekwa katika maduka ya uuzaji bidhaa, benki na vituo vya treni.
Hospitali moja inamipango ya kuajiri roboti zaidi kwa miaka 10 ijayo.
Baadhi ya wataalamu wamehoji umuhimu wa roboti za kijamii kama vile Pepper.

Image copyrightAFP
Image captionRoboti

Kampuni ya softbank, iliyomtengeneza Pepper na kampuni ya Aldebaran wamepata faida kubwa kwa ubunifu huyo haswa kutoka Japan.
Roboti hiyo inaurefu wa kina futi nne na inauwezo wa kutambua sauti za binadamu kwa lugha 20 na inauwezo wa kubaini iwapo inazungumza na mwanamume, mwanamke au mtoto.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP