Tikoooooooo
STAA wa filamu na Bongo Fleva, Tiko Hassan amepania kutengeneza video kali itakayoifunika ile ya Chura ya msanii Snura Mushi iliyopigwa marufuku kuoneshwa.
Akichonga na Chanzo cha habari hiziTiko alisema anaandaa video kali ya wimbo wake wa Watu ambayo ndani yake kutakuwa na kukata mauno ya kufa mtu kuliko ile ya Snura.
“Itakuwa ni video ambayo haijawahi kutengenezwa hapa Bongo, ni hatari yaani, ninachowaomba mashabiki ni kuisubiri kwani ‘soon’ itashuka,” alisema msanii huyo na kuongeza kuwa hata hivyo, haitakuwa iliyokosa maadili.
Stori: Gladness Mallya