Vikosi vya usalama nchini Ethiopia vimewaua zaidi ya watu 400 wakati wa maandamano ya hivi majuzi ya kupinga serikali.
Shirika la haki za binadamu lenye makoa yake nchini Marekani HRW, kwenye ripoti ya maandamano ya jamii ya Oromo ,limetoa orodha ya majina ya zaidi ya watu 300 linalosema waliuawa.

Serikali imethibitisha kuwa waandamanaji walikufa, lakini pia imesema kuwa HRW haikusema ukweli kuhusu idadi.

Image copyrightAFP

Maandamano hayo yalianza kutokana na hofu kuwa mpango ya kupanua mji wa mkuu Addis Ababa kwenda eneo la Oromia ungesababisha kuhama kwa wakulima wa Oromo.
Hata hivyo serilia ilitupilia mbalia mpango huo ambao ungeanza mwezi Januari.