Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifanya usafi katika mazingira ya Hospital ya Temeke mwishoni wa wiki iliyopita katika maadhimisho ya shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke ambapo wafanyakazi hao walifanya usafi katika mazingira ya hospitali hiyo wakishirikiana na Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na timu yake


Usafi ukiendelea katika mazingira ya Hospitali ya Temeke ambapo pia wafanyakazi wa SBL mapema wiki iliyopita ikiwa ni moja ya shughuli za kijamii pia walijitolea kuchangia damu na kupima afya zao  katika Hospitali hiyo


Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja mapema wiki iliyopita mara baada ya kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Temeke 




Meneja wa Usalama na Afya kazin wa SBL Bwana David Mwakalobo akimkabidhi vifaa vya usafi Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke




Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia Serengeti (SBL) akichangia damu ambapo  zoezi hilo la kuchangia damu liliambatana na shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke



Dar es salaam ,3 Juni ,2016 ;Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) leo
wamechangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam ikiwa ni moja
ya mpango ya kampuni  kusaidia sekta ya
afya nchini.

Uchangiaji wa damu ni moja ya shughuli za kusaidia jamii zinazoendana
sambamba  na wiki ya afya na usalama kazini
kwa kampuni hii,tukio hili linalofanywa kila mwaka likilenga viwanda vya bia na
vinywaji vikali kuongeza ufahamu kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kuzingatia
usalama sehemu za kazi.

Akiwashukuru wafanyakazi wa SBL kujitokeza kwa wingi kuchangia damu
Meneja Uzalishaji wa kiwanda cha Dar es salaam Alice kilembe alisema zoezi hili
linaenda sambamba na mipango ya kusaidia jamii na lengo ikiwa ni kusaidia   kuboresha afya zao.

“Tunapenda kuwashukuru wafanyakazi wote kujitokeza kuchangia damu
.Tunaamini msaada huu wa damu utasaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji na
pia kusaidia kuboresha afya za watu wetu “alisema Kilembe

Mapema leo Kiwanda cha Serengeti cha Dar es salaam wameshiriki pia katika
usafi wa mazingira kuzunguka katika maeneo ya Temeke jambo ambalo meneja uzalishaji
wa kiwanda alisema ni “kuitikia wito wa serikali wa kuhakikisha usafi katika
maeneo ya wazi”

Kwa mujibu wa Kilembe SBL haijakumbwa na matatizo katika maeneo ya kazi
kwa zaidi ya miaka minne ikiwa ni matokeo ya mafunzo ya mara kwa mara kwa
wafanyakazi na tahadhari zinazochukuliwa zinazofanya kampuni kukidhi viwango ya
kimataifa vya usalama katika mazingira ya
kazi.