MKALI katika gemu la muziki Bongo, Banana Zorro amesema kuwa kujitenga na masuala ya skendo ndiko kumemfanya asisikike mara kwa mara kwenye media, jambo ambalo halimnyimi usingizi maana mbali na kusikika huko kupitia kwenye bendi yake ya B Band anapata kipato kizuri kinachompiga tafu kimaisha.
Akistorisha na Ebwana Dah, Banana alisema kuwa sababu za kujitenga na skendo ni kutokana na kuiheshimu ndoa yake maana hadi sasa ana muda wa miaka kumi akiwa ni mume wa mtu!
“Nafahamu kuwa skendo ndizo zimenipoteza kwenye media lakini sijali, napiga shoo kila mara na bendi yangu jambo ambalo linanifanya niishi kibosi kuliko hata baadhi ya hao wanaosikika kwenye media mara kwa mara kutokana na skendo zao,” alisema Banana.
0 Comments