Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 22, 2016

MAMA YAKE HAMISA MOBETO,AWASHUKIA VIKALI,AMAINDI MWANAYE KUTUKANWA


MAMA mzazi wa mwanamitindo ‘hot’ Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga kwa mara ya kwanza anatengeneza ‘headline’ baada ya kufungukia madai ya mwanaye ‘ku-date’ na Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha kuambulia mitusi.


Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mama huyo alisema hakuna kitu kinachomuuma kama mwanaye kutukanwa mitandaoni kwa kuhusishwa kimapenzi na Diamomd jambo analoamini halina ukweli.
“Mimi kama mzazi naumia kuona mwanangu anatukutanwa kwa mambo ambayo hayana ukweli, hana uhusiano na Diomond jamani,” alisema mama huyo.
Hamisa juzikati alioga matusi kutoka kwa Team Zari baada ya video mbalimbali kumuonesha akipewa nafasi ya mbele zaidi kwenye ‘bethidei’ ya mama Diamond, kuliko Zarinah Hassan ‘Zari’ jambo lililotafsiriwa kuwa huenda Hamisa kafanya mapinduzi.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP