Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 28, 2016

DRC:Jaji aliyemhukumu Katumbi adai alishinikizwa

Jaji mmoja wa mahakama ya juu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekiri kuwa alishinikizwa na majasusi na wakuu wake katika idara ya mahakama kumpata na hatia kiongozi wa upinzani Moise Katumbi.

Jaji Chantal Ramazani alikuwa miongoni mwa jopo la majaji waliokuwa wakisikiza kesi hiyo dhidi ya katumbi ambaye hakuwa mahakamani.
Jopo hilo la majaji lilimpata Katumbi na hatia na kumhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kuuza mali kinyume cha sheria.
Bi Ramazani, sasa hivi yuko mafichoni.
Anaamini kuwa kauli hiyo ya mahakama ilikusudia kumzuia kiongozi huyo wa upinzani katika kinyang'anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Uchaguzi mkuu nchini humo umepangwa kufanyika mwezi Novemba.
Haikuwezekana kupata maoni ya viongozi wake mkuu wa idara ya mahakama wala idara ya ujasusi nchini humo kuhusiana na madai ya jaji huyo.
Bwana Katumbi kwa upande wake anasema kuwa anakusudia kurejea nyumbani DRC mwishoni mwa juma.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP