Kwa wale wanaopendelea kuvaa suruali hasa za jeans, sasa hivi imeingia fasheni mpya ambayo kwa wale wasio wajanja bado wanaishangaa. Hizi ni zile jeans ambazo zinaitwa Jeans Mraruko. Najua unawaona wadada na wakaka wengi wakiwa wamezivaa.
Aidha, wapo wanaoziponda kiaina wakisema eti wanaovaa suruali hizo ni vichaa wasafi, kwamba ni sawa na wale vichaa ambao suruali zao zimechafuka lakini zimechanika kwa staili hiyohiyo.
Wanaosema maneno hayo wala hutakiwi kuwasikiliza, kama kweli wewe ni mtu wa kwenda na wakati, jeans hizo zinakuhusu. Wanaovaa kwanza wanaonekana wajanja, wanaokwenda na wakati lakini pia zinawatoa chicha kama unavyowaona mastaa wakubwa wa nje na ndani ya Bongo kama vile Jokate, Kidoa, Masogange, Wema, Lulu, Kim Kardashiana, Amber Rose, Rihanna na wengine wakiwa wamezivaa, wewe unasubiri nini?
0 Comments