Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 23, 2016

Kisa kushuti malaika alia kama mtoto

MALAIKA

MWANADADA anayeanza kujivunia mashabiki wengi kwenye Tasnia ya Muziki Bongo, Diana Exavery ‘Malaika’ amefunguka kuwa amewahi kulia kama mtoto kisa vikwazo vilivyokuwa vinajitokeza wakati anashuti kichupa cha Wimbo wa Sare.
Akichonga na Burudani Mwanzo Mwisho (BMM), Malaika alisema vikwazo hivyo vilikuwa ni pamoja na mvua kubwa kunyesha, jambo lililosababisha kukaa muda mrefu lokesheni, zaidi ya siku tano na kulazimika kutumia gharama kubwa ambayo hakuwa amepanga kiasi kwamba baadaye alifahamu asingefanikiwa kumaliza zoezi hilo.
“Kila siku mvua ilikuwa inanyesha kuliko kawaida sehemu tuliyopanga kufanyia video hiyo na mbaya zaidi tulikuwa tumefikia hoteli, halafu kuna vitu tulikuwa tunaandaa lokesheni kama mabango yakawa yanalowana, kiukweli ilikuwa ni kazi ngumu, ile siku ya tano niliendesha gari langu na kwenda sehemu nikaanza kulia sana,” alisema Malaika na kumalizia kuwa;
Baada ya kulia, alijipa moyo kuwa kila kitu kingekwenda sawa na kweli ikawa hivyo.
Stori: BMM, RISASI JUMAMOSI
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP