Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 23, 2016

Vee Money, Iyobo ndani ya AFRIMMA 2016

vee moneyVanessa Mdee ‘Vee Money’

OKTOBA 15, 2016 ndani ya Ukumbi wa The Black Academy Of Art and Letters, uliyopo Dallas huko Texas, Marekani kunategemewa kugawiwa Tuzo za Afrimma (African Music Magazine Awards), zinazowashirikisha wasanii mbalimbali kutoka Afrika.
Huu utakuwa msimu wa tatu tangu tuzo hizi zianze kutolewa ambapo katika miaka ya 2014- 2015 zimekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa na muitikio mzuri wa watu wanaojitokeza kuonesha ushirikiano kwa kupiga kura na kuhudhuria wakati ambao tuzo hizo hutolewa.
Moses-Iyobo-at-Jembeka-Festival-2016Moses Iyobo.
Katika tuzo za mwaka huu hali ya ushindani inaonekana kuongezeka katika vipengele wanavyopatikana mastaa wakubwa Afrika wakiwemo Wizkid, Mr Flavour, Davido, Sarkodie na Aka baada ya sura mpya za wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa Afrika kuingia ambao ni pamoja na Falz, Mr. Eazi, Locko na Bisa Kdei.
Kwa upande wa Tanzania, katika tuzo hizi imechafua kwenye vipengele mbalimbali ikiwakilishwa na wasanii zaidi ya saba ambao miongoni mwao ni Vanessa Mdee ‘Vee Money’, DJ D-Ommy , Tud Thomas na Moses Iyobo.Stori: BMM, RISASI JUMAMOSI
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP