Timu ya Taifa ya Ureno imeweza kunyakua ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) baada ya kuwagaragaza wenyeji wa Mashindano hayo Timu ya taifa ya Ufaransa kwa kichapo cha bao 1-0 lililotiwa kimiani mnamo dakika ya 109 ya mchezo na Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Swansea, Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes baada ya kuachia shuti kali umbali wa mita 25 uliomshinda Mlinda mlango wa Timu ya Ufaransa, Hugo Lloris na kuingia kimiani.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ureno wakishangia kwa pamoja ushindi walioupata kupitia kwa Mshambuliaji, Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji wa Mashindano hayo, Ufaransa, uliochekwa katika uwanja wa Stade de France.