Mkuu wa polisi katika mji wa Dallas amesema wamepata ushahidi kuwa Micah Johnson alifanya majaribio ya kulipuwa vilipuzi.
Kabla ya kuuawa Ijumaa asubuhi, Johnson aliwaambia polisi amekasirishwa na matukio ya hivi karibuni ya mauaji dhidi ya watu weusi yanayofanywa na polisi.
Maafisa watano wa polisi waliuawa katika shambulio hilo