Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 2, 2016

Makonda Atangaza Msako kwa ‘Mashoga’ Dar

MakondaMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Dar es Salaam
KUTOKANA na kuongezeka kwa vitendo vinavyoashiria kuwepo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza operesheni ya kuwasaka wanaume wanaojihusisha na tabia hiyo mbovu ya ‘mashoga’ jijini humo ilihali wakijua ni kinyume cha sheria za nchi.
Makonda amesema vitendo hivyo vimeanza kuongezeka jijini humo na lengo lake ni kuwaokoa watoto wasiige mambo hayo yanayoonekana kukua kwa kasi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema, “hili ni tatizo linalokua kwa kasi sitaruhusu liendelee katika mkoa wangu, nitawasaka popote walipo”.
“Hata hapa bandari wanaweza kuwapo mashoga wafichueni, mkiona mtu ana tabia za ajabu ajabu mfichueni, tutashughulika nao”.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP