Baadhi ya Marais Wastaafu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wadau mbalimbali kwenye mkutano huo Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili umewajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali.
Mtoa mada mkuu wa mkutano wa 'African Leadership Forum' Bw. Sipho Nkosi, ambaye ni mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti Mstaafu wa Chemba ya Madini kutoka Afrika Kusini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Bw, Nkosi ni bilionea watatu mweusi anayeongoza kwa utajiri Afrika Kusini.
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akichangia moja ya mada katika Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) ulio anza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali.
Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akichangia moja ya mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) wa siku mbili,unaondelea hivi sasa katika hoteli Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,ambapo Mabalozi kutoka nchi mbalimbali pamoja na Wadau wengine wameshiriki.
Waziri wakuu wa Wastaafu katika awamu mbalimbali nchni Tanzania,pichani kulia ni Mh David Cleopa Msuya,Mh John Samuel Malecela pamoja na Mh.Salim,Ahmed Salim wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili umewajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali.
Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI walioandaa Mkutano MKuu wa UONGOZI wa 2016 sambamba na Waratibu wa Mkutano huo Kampuni ya MONTAGE wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo asubuhi ndani ya hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako ndiko mkutano huo unafanyika.
Mkutano ukiendelea
Baadhi ya Mabalozi na Wadau wengine wakifuatilia yanayojiri katika mkutano huo unaoendelea hivi sasa ndnai ya hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijni Dar
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano huo.
0 Comments