Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 28, 2016

Madai Jack Chuz aachika tena

JACKYWACHUZII.jpg
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Steven Pentezel ‘Jack Chuz’ aliyekuwa akiishi na mumewe, Gadna Dibibi anadaiwa kuachika kwa mara ya pili.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na staa huyo, ndoa yao imekuwa na migogoro mara kwa mara na kwamba safari hii jamaa kamuacha jumla.
“Ubuyu ulioonyooka ni kwamba, yule Jack Chuz kwa sasa ameachika na safari hii sidhani kama watarudiana tena maana jamaa kamchoka,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyaka ubuyu huu, Showbiz Xtra ilimvutia waya Jack ambapo alifunguka;
“Jamani, jamani! Kweli nimeamini hakuna mtu anayependa maendeleo ya mwenzake, sijaachika na haitakuja kutokea. Katika ndoa lazima kuwe na migogoro ya hapa na pale ila si kuachika, watu waache kujadili ndoa yangu,” alisema Jack.
Wawili hao walioana mwaka 2013, tangu hapo wamekuwa wakikwaruzana ambapo mwaka jana walidaiwa kumwagana na staa huyo akihama nyumbani kwake, Sinza-Mori na kuhamia hotelini.IMELDA MTEMA
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP