Waislamu kote duniani wanajiandaa kusherehekea sikukuu ya Idd ul fitr siku ya Jumatano, hiyo itakuwa kilele cha mwezi mzima wa ibada pasi na kula wala kunywa kuanzia alfajiri hadi jioni.
Saumu ambayo hudumu kwa takriban siku thelathini ni moja ya nguzo kuu za dini hiyo.
Katika kipindi hicho chote mtu mwenye akili zake hutakikana kujizuia kula na kunywa iliangalau aelewe jinsi wale ambao hawana uwezo wa kununua chakula huhisi.
Aidha mja huweza kufungua kwa masharti fulani.
Kama ni mgonjwa, ama ni mwanamke anayenyonyesha ama ambaye yuko kwa hedhi.
Lakini kuna jamii fulani huko Senegal ambao wao ni waislamu ila hawajakuwa wakifunga nao ni watu wazima na akili zao.
Sababu yao kukosa kufunga ni nini ?
Wafuasi hao wa dhehebu la Baye Fall wanafuata itikadi ya Sufi.

Image copyrightGETTY
Image captionSaumu ambayo hudumu kwa takriban siku thelathini ni moja ya nguzo kuu za dini hiyo.

Imani yao inawataka wajinyime na kuwalisha jamii wasiojiweza.
Mwandishi wa BBC aliyeko katika mji wa Touba
Wakati wa ramadhan wafuasi wa dhehebu hilo hupika chakula na kuwapa futari wale waislamu wanaofunga kula na kunywa.
Kulingana nao thawabu wanazopata kwa kuwalisha wale wanaofunga kula na kunywa ni kubwa mno kuliko kujenga misikiti 1000.
Mara nyingi utaona umati wa watu wakiwa wamebeba sinia kubwa kubwa za vyakula mbalimbali wakiwaandalia wale wanaofunga.
Wakati huu wa ramadhan bila shaka wanasikitika wakati wao wa kuvuna amana umekamilika haraka.