Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
(kushoto) akiwapungia wananchi wakati alipomkaribisha Mke wa Rais wa
Rwanda Mama Janeth Kagame katika Ofisi zake wakati wa Ziara ya Rais wa
Rwanda Mh. Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisaini kitabu cha
wageni wakati alipotembelea ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mama Janeth Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam
ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa
nchini .

Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisikiliza kwa
makini shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli wakati alipotembelea ofisi hizo ikiwa ni sehemu ya ziara
ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mke wa Rais wa
Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea
ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa
Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiagana na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame
(kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli
ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Benjamin Sawe - Maelezo