Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe (wa pili kulia), akizungumza katika Uzinduzi wa Motisha Mpya ya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika jana Jijini Mwanza.

Wengine ni Joseph Mwaigombe ambae ni Meneja Mauzo na Usambaji wa Kampuni ya TDL Kanda ya Ziwa (wa kwanza kushoto), Deogratius Nabigambo ambae ni msambazaji wa vinywai vikali eneo la Ngara na Biharamulo mkoani Kagera (wa pili kushoto), na Martha Bangu ambae ni Meneja wa chapa yaa Konyagi (wa kwanza kulia).


Katika Motisha (Promotion) hiyo, wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi wataingia katika droo ya kushindania magari mawili ambapo kila moja lina thamani ya Shilingi Milioni 46 pamoja na zawadi mbalimbali ikiwemo kitita cha fedha.

Zawadi za Motisha hiyo zitatolewa kwa Wasambazaji na Wauzaji wote nchini watakaouza katoni za Konyaji kuanzia 400 hadi 30,000 kwa mwezi.
Na BMG
Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe (kushoto), akizungumza katika Uzinduzi wa Motisha Mpya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika jana Jijini Mwanza. Kushoto ni Martha Bangu ambae ni Meneja wa chapa yaa Konyagi 
Deogratius Nabigambo ambae ni msambazaji wa vinywai vikali eneo la Ngara na Biharamulo mkoani Kagera (kushoto) akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema akibahatika kushinda zawadi ya gari itamsaidia katika shughuli zake za usambazaji wa Kinywaji cha Konyagi ambapo aliwasihi wasambazaji wengine kuitumia fursa hiyo kwa kuongeza mauzo yao ili kuingia katika droo hiyo ya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi. Kulia ni Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe
Wasambazaji na wauzaji wa vinywaji vikali Kanda ya Ziwa wakiwa katika Uzinduzi wa Motisha (Promotion) ya  Nunua, Uza, Shinda na Konyagi uliofanyika jana Jijini Mwanza.
Ufafanuzi ukitolewa kwa Wasambazaji na Wauzaji wa Vinywaji Vikali Kanda ya Ziwa, katika Uzinduzi wa Motisha Mpya ya Nunua, Uza, Shinda na Konyaji uliofanyika jana Jijini Mwanza
Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe, akizungumza na Wanahabari katika Uzinduzi wa Motisha Mpya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika jana Jijini Mwanza.