Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa chama hicho.


Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake kumsalimia.

Mketo ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni leo Dar es Salaam leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul alipo kuwa  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.

"Tunasema sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake" alisema Mketo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
alisema chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa jeshi hilo wakati wowote litamkamata  Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea  wafuasi wake ili waichukie serikali iliyopo madarakani.

Alisema baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP  Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mazrul  alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.

Alisema jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila ya kuwafikisha mahakamani.

Mazrul alisema  hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi.