Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete
akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya
kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika
wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi wakimsikiliza Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete katika hafla ya
kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika wilaya
ya Bagamoyo. 


Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na Mke wa Rais
Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete,mama Salma Kikwete, katika hafla ya
kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika
wilayani Bagamoyo,wengine ni wabunge wa mkoa huo wakimsalimia
Mwenyekiti huyo mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi mbalimbili wa mkoa wa Pwani.(Picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Na David John Pwani 


MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete
amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi
ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais
ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo
alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia
flaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.

Amesema wakati
akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani
Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye
Komputa.

Dkt.Kikwete ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika
hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka
mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alisema.anashukuru
Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na kwamba amemaliza salama na
ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi.
Akikumbuka mchakato wa mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo
mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .


"Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na
wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi"amesema Dkt.Kikwete
.Aidha amesema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu
ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza
hata nchi jirani.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi
amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa
yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na
Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojalibu kupeleka
maendeleo Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa
hawana haki.

Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha
fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara
ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na
hadi kufikia wabunge kulumbana.

Amesema hata hivyo anashukuru
kwamba amemaliza salama na Kwa Bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana
ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga
mkono.
Wanachana

Wanachama wa Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo wamejitokeza Kwa wingi kumkaribisha nyumbani
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho Dkt.Jakaya Kikwete katika sherehe
zilizofanyika wilayani Bagamoyo. Wanachama hao ambao walitoka katika
wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho
mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga walimuaga na kumkaribisha
Kwa nyimbo mbalimbali.