Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU juzi siku ya jumamosi 16 Julai 2016 ilifanikiwa kwa mara nyingine kudhiirishia ulimwengu kwa kuwatia kiwewe washabiki katika onyesho kubwa la muziki lilifanyika katikati ya mji wa Bayreuth,ujerumani ya kusini,bendi ikiongozwa na mkuu wake Kamanda Ras Makunja ilikwea jukwaani majira ya saa tatu usiku na kuunza kudatisha maelfu ya washabiki ,watayarishaji wa onyesho hilo kubwa kampuni ya Tropical Internaiment wamesema haijawai kutokea bendi kama hii Ngoma Africa band ambayo mudundo wake umewachangaya akili watu wote hapa!!