Kwa mtazamo wa wengi radi haiwezi kupiga mti mmoja mara mbili.,,, lakini kwa mwanamke mmoja nchini India hilo ndilo lililomkuta.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili.

Image copyrightREUTERS
Image captionMiaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani.

Miaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani.
Sadfa ni kwamba binti huyo aliyetorokea mji tofauti wa Rohtak ulioko katika jimbo la Kaskazini la Haryana alishikwa na kubakwa tena juma lililopita.
Alikuwa akitembea barabarani kisha akatekwa nyara na watu ambao nusura wamnyonge.
Alinusurika kufa lakini alichokipitia ni cha kutamausha sana.

Image copyrightREUTERS
Image captionBinti huyo alibakwa kwa mara ya pili na kutupwa kichakani.

Binti huyo alibakwa na kutupwa kichakani.
Kwa bahati nzuri msamaria mwema aliyekuwa akipita eneo hilo alimsikia akitoa sauti hafifu na kumpeleka hospitalini alikotibiwa hadi akarejesha afya yake.
Alipopata afueni alisema maneno yaliyoibua hasira miongoni mwa jamii.

Image captionBinti huyo alibakwa na kutupwa kichakani.

''Nilikuwa nikitembea barabarani nikitoka chuoni kuelekea nyumbani kisha nikawaona walewale wanaume walionibaka huko Rohtak.
Nilishtuka na kuhofia maisha yangu. Walishika na kujaribu kuninyonga.walinieleza kuwa watawaua babangu na kakangu.''

Image captionMamia ya wenyeji wa mji wa Rohtak, wameandamana wakitaka serikali iwachukulie hatua kali washukiwa hao wa kosa hilo la kinyama.

Sijui walikonipeleka kwa sababu nilipoteza fahamu ila ninachokijua ni kuwa walikuwa wale wale walionibaka miaka mitatu iliyopita.'' binti huyo kutoka jamii maskini aliiambia runinga moja ya kitaifa nchini India.
Familia yake inasema kuwa washukiwa hao walikuwa wakiwashinikiza kukomesha mashtaka dhidi yao lakini binti yao akakataa kata kata.
Sasa polisi wametumwa huko kuwasaka watuhumiwa hao.
Mamia ya wenyeji wa mji wa Rohtak, wameandamana wakitaka serikali iwachukulie hatua kali washukiwa hao wa kosa hilo la kinyama.