Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 25, 2016

Petit, Esma sasa hadi kiama!

petitmmanEsma Platnumz na mumewe, Hamad Manungwa ‘Petit Man’
STORI: Imelda Mtema, Wikienda
Dar es Salaam: Mume wa dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz, Hamad Manungwa ‘Petit Man’ amefunguka kuwa watu wanachonga juu ya uhusiano wake na mzazi mwenzie huyo lakini ndiyo ameshanasa hadi kiama.
esma-4Akizungumza na Wikienda, Petit Man alisema kuwa ameona bora kukaa na kutulia na mwanamke wake huyo ambaye wamezaa mtoto mmoja wa kike waliyempa jina la Taraj kwa sababu kwingine ni kujitafutia ‘stress’ ambazo hazina sababu za msingi.
petit“Najua kuna watu wanachonga sana juu ya uhusiano wangu na Esma lakini kiukweli wanune, wanenepe, wavimbe lakini ndiyo nimeshamaliza hapo hadi kiama,” alisema Petit aliyemwagana na Esma kisha kurudiana.
Aliongeza kuwa, hivi sasa wameungana na kuongeza nguvu zaidi ya kufanya kazi za burudani ili kuandaa maisha mazuri ya mtoto wao.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP