Vikosi vya usalama nchini Uturuki vinasema kuwa zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi wamefutwa kazi, kufuatia jaribio la mapinduzi lililozimwa wiki iliyopita.
Runinga rasmi ya serikali nchini Uturuki- Anadolu, inasema kuwa maafisa wengine waliokamatwa ni pamoja na majenerali wakuu wa kijeshi.
Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa.

Image captionFethullah Gulen amekanusha madai ya kuchochea mapinduzi

Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa hao wanalaumiwa kwa kuwa na uhusiano na mapinduzi hayo ambayo serikali inadai kuwa yalipangwa na kiongozi wa dini aliyeko uhamishoni nchini Marekani- Fethullah Gulen.
Msako dhidi ya maafisa wa usalama waliohusika na mipango ya kuipindua serikali juma lililopita nchini Uturuki, unaendelea.

Image copyrightREUTERS
Image captionKituo cha mafunzo ya wanajeshi wa angani mjini cha Istanbul, kilivamiwa na maafisa kukamatwa.

Usiku wa kuamkia leo na mapema Jumatatu alfajiri, zaidi ya maafisa elfu nane 8,000 wa polisi walikamatwa kushauriwa kuwasilisha bunduki zao na kusimamishwa kazi.
Kituo cha mafunzo ya wanajeshi wa angani mjini cha Istanbul, kilivamiwa na maafisa hao kukamatwa.
Waendesha mashtaka wameanza kuwahoji kinara mkuu wa jaribio hilo la mapinduzi ambaye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la angani Akin Ozturk, ambaye ni miongoni mwa makamanda wakuu 100 waliokamatwa.

Image copyrightEPA
Image captionTakriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa.

Maafisa wanane wa kijeshi walioingia nchini Ugiriki kwa kutumia Helikopta, wamefikishwa mahakamani katika mji ulioko mpakani wa Alexandrou-poli, ili kushtakiwa kwa kuingia nchini humo bila idhini.
Uturuki imeomba Ugiriki kuwarejesha nyumbani ili kushtakiwa, lakini mawakili wao wameomba idhini ya uhamiaji.