Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kutuma kikosi maalumu cha kimataifa nchini Burundi kujaribu kutuliza ghasia na ukiukaji wa haki za kibinadamu ambao umekumba taifa hilo la Afrika ya Kati kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Baraza hilo liliidhinisha pendekezo lililowasilishwa na Ufaransa, lililopendekeza zaidi ya maafisa wa usalama 228 wawe nchini humo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Image copyrightGETTY
Image captionRais Pierre Nkurunziza

Awali Serikali ya Burundi ilikuwa imesema kuwa haitawakubali zaidi ya polisi 50.
Zaidi ya watu 500 wameuawa wengi wao katika mauaji bila kufikishwa mahakamani.
Mauaji hayo yamelaumiwa maafisa wa polisi.

Image copyrightREUTERS
Image captionGhasia nchini Burundi

Ghasia zilianza nchini humo wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mipango yake ya kutaka kugombea urais katika awamu ya tatu, ambapo alifanya hivyo na kushinda.