Hillary Clinton anawania urais akiungwa mkono na Barrack Obama.
Obama alimuidhinisha rasmi katika kongamano la chama cha Democrat.
Image copyrightREUTERSImage captionObama na Clinton
''Hakujakuwa na mwanamume au mwanamke ,sio mimi wala Bill Clinton hakuna aliyefuzu zaidi ya Hillary Clinton'', aliuambia umati wa watu.
Walikumbatiana na kuonekana kwamba walikuwa marifiki wa jadi .Lakini haijakuwa hivyo .
Image copyrightGETTYIMAGESImage captionClinton
Alipogundua kwamba huenda asishinde dhidi ya Obama miaka iliopita bi Clinton alimfanyia kampeni bwana Obama.
Aliposhinda urais Obama alimteua bi Clinton kama waziri wa maswala ya kigeni.
Image copyrightGETTYImage captionObama na Clinton
Haikuwa rahisi kwani baadhi ya wasaidizi wake walishindwa kujirekebisha ili kuingiliana na uongozi wa Obama.
|
0 Comments