Polisi nchini Marekani wanasema watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika shambulio lililoekelezwa katika kilabu cha usiku jimbo la Florida.
Watu wengine kadha wamejeruhiwa.

Kisa hicho kimetokea katika mji wa Fort Myers, ambalo kilabu kimoja kilikuwa kimeandaa tamasha kwa ajili ya vijana.
Majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa kutumia magari ya kuwabeba wagonjwa.
Polisi bado wanajaribu kubaini chanzo cha ufyatuaji risasi huo.
Mtu mmoja amezuiliwa na anahojiwa.