Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya






Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali





DcNdejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali

Na Mathias Canal, Singida




Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru
katika kituo cha Afya cha Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani
humo kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini
kupatiwa tiba.



Huu ni muendelezo
wa ziara za kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya
kupunguza na kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na
wananchi wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya
hususani sekta ya Afya.



Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho
cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali,
wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na
kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea
kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.



Licha
ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango chini ya usimamizi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
kuhudumu katika Wilaya hiyo.



Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe
Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze
kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake
mwenyewe.



Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa Kituo cha afya Mlali
kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya umma ili kuendelea kutoa
huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila Mtanzania anayefika katika
Zahanati hiyo.



Kwa upande wa wananchi waliofika kupatiwa huduma
kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema kuwa huduma
zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa huku
changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto kwani
hawapati huduma hiyo kwa wakati.



Sambamba na hayo Dc Ndejembi
ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi
wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia na
kuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana ya
HapaKaziTu kwa vitendo.