Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake
 


Familia ya
marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura
pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na
Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa
upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika
kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo


(pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi,
kwa ajali ya gari.


Familia
inapenda kuwashukuru kipekee Wakwe wa marehemu - familia ya Mzee Edriss
Mavura;  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Prof Elifas T. Bisanda pamoja na
uongozi wa chuo na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT); 



Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Afya duniani (WHO) Uganda na
Tanzania; Dr Harvinder Palaha wa Aga Khan Hospital, na madaktari wenzie,
wauguzi na wafanyakazi wote wa Aga Khan Hospitali kitengo cha wagonjwa mahututi
(ICU); 

Mzee wetu Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia
yake; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi;
Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania na Bw. Ziya Kaharan, Balozi wa Heshima wa
Tanzania nchini Uturuki; Prof. Fatmahan Atalar, Mkurugenzi wa MUHAS Genetic
Laboratory ya Chuo Kikuu cha Muhimbili; Wanajumuiya wa Ikungi Development
Association (IDEA); Umoja wa Wanafunzi waliosoma Uturuki, Masheikh wa Dar es
Salaam na Ikungi; na Majirani wote wa Dar es Salaam na Singida.

Kwa kuwa
si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, tunaomba wote mlioguswa na msiba huu
mpokee shukrani zetu za dhati.

Tunapenda
kuwataarifu kuwa Dua ya arobaini (40) ya marehemu itasomwa Jumamosi, tarehe 03
Septemba 2016, Makiungu-Ikungi, Singida, saa 5 asubuhi Wote mnakaribishwa.


INNA
LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUUN