Safari ya mtalii mmoja kutoka nchini China aliyeenda kutalii Ulaya imeishia kwenye moja ya kambi za kuhifadhia wakimbizi nchini Ujerumani baada ya kuomba usaidizi kutoka kwa mamlaka nchini humo.

Mtalii huyo alipoteza pochi akiwa likizo mjini HeidelbergImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionAlipotoa taarifa polisi alishindwa kueleweka kutokana na ugumu wa lugha

Mtalii huyo alipoteza pochi akiwa likizo mjini Heidelberg na alipotoa taarifa polisi alishindwa kueleweka kutokana na ugumu wa lugha.Badala yake akatakiwa kujaza fomu za kuomba hifadhi kwa siku 12 kwenye kambi ya wakimbizi iliyopo mamia ya kilomita kutoka mjini.

Alama za vidole huchukuliwa kwa wahamiaji pindi wanapoingia UjerumaniImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionAlama za vidole huchukuliwa kwa wahamiaji pindi wanapoingia Ujerumani

Mkanganyiko ulimalizwa na mfanyakazi mmoja wa shirika la misaada,programu ya kutafsiri ya Kichina na baadhi ya watalii waliokuwa wakielekea nchini Italia kwa mapumziko